Suche einschränken:
Zur Kasse

Hujafa Hujaumbika

Kagwa, F. M.

Hujafa Hujaumbika

Mwanga, almaarufu 'Fumo', ni kijana mdogo ambaye hana hakika na asili walafasili yake. Yeye ni msi baba, msi mama. Anachokifahamu ni kwamba'aliokotwa' kutoka katika makao ya mayatima. Licha ya kuwa yeye ni kiokote, mlezi wake anampa kila kinachostahili kwa mtoto mwenye wazazi wote.Hali inapoonekana kutakata, msiba baada ya msiba unabisha. Mlezi wake wapekee ambaye anamjua kama 'mama' anapigwa kalamu. Nyumba yao inauzwakwa wenye nacho. 'Dada yake' Fumo ananajisiwa na kubaki hali mahututikatika mshikemshike wa kufurushwa kutoka kwa nyumba yao na wahuniwalioletwa na mmiliki mpya. Baadaye, mlezi wa Mwanga anafunguliwamashtaka ya kusingiziwa ili asiweze kufuata kesi ya kufutwa au kufurushwakutoka kwa nyumba yake. Mwanga na 'familia' yake wanajipata katika mitaaya vitongoji duni. Choo ni cha 'kurusha fataki' na bafu ni upenuni. Hamna staratena!Akiwa shuleni, Mwanga anafanya bidii ya mchwa na kupita vyema, lakinimikosi bado haimwachi akapumua. Huku akicheza na watoto wengine, anajipata amekanyaga kilipuzi na kupoteza mguu wake. Lakini bidii yake nakudura za Mwenyezi Mungu vinamwezesha kuwa mwanasheria nguli. Azmayake sasa ni kutetea haki licha ya kilema chake. Kumbe kufa si kufariki, kufani kuoza utumbo!Hii ni riwaya ya kusisimua yenye kutia matumaini katika jamii iliyotamaukakutokana na matatizo mengi yanayoletwa na ufisadi na kupotoka kwamaadili.

CHF 40.90

Lieferbar

ISBN 9789966315687
Sprache swa
Cover Kartonierter Einband (Kt)
Verlag For Our Sun Publishing
Jahr 20180202

Kundenbewertungen

Dieser Artikel hat noch keine Bewertungen.